Welcome to Souq commerce Store !
kilimo bora cha nyanya

kilimo bora cha nyanya

Size :
(0 customer review)

1. Kuandaa Kitalu cha Nyanya Mambo muhimu ya kuzingatia:
 

  • Kitalu kiwe karibu na maji ya kutosha na ya kudumu 
  • Kiwe sehemu iliyowazi na yenye udongo ulio na rutuba ya kutosha 
  • Eneo la kitalu kama ni kubwa liwe tambarare au na mwiinuko kidogo ili kuepuka maji yasituame kwenye kitalu, mtelemko ukiwa mkali sana nao sio mzuri kwani husababisha mmomonyoko wa udongo. 
  • Kitalu kiwe sehemu ambayo haikuwa na zao la nyanya au viazi  mviringo (au mazao ya jamii ya nyanya k.m. mnavu, biringanya n.k.) 
  • Kiwe sehemu ambayo ni rahisi kupata huduma zote muhimu kwa urahisi, ikiwa ni pamoja na uhamishaji wa miche kwenda sehemu nyingine. Pia kurahisisha usambazaji wa miche kwenda sehemu nyingine. 

2. Kuandaa Matuta ya Kusia Mbegu za Nyanya Aina ya matuta:

– matuta ya makingo (sunken seed bed) 
– matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed bed) 
– matuta ya kawaida (flat seed beds) 
 
•Mbegu zinaweza pia kusiwa kwenye vyombo mbali mbali au sehemu nyingine mbali na matuta, kwa mfano; kwenye vikasha vya mifuko ya nailoni, masago ya      migomba, vijisanduku vidogo vilivyo jazwa udongo n.k. 
– Wakati wa kujaza udongo kwenye vyombo hivyo sharti udongo huo uwe na rutuba ya kutosha. 
– Udongo mzuri ni ule ulio changanywa vizuri na samadi, mbolea vunde au mboji ya kutosha. 

3. Mambo Muhimu ya Kuzingatia wakati wa Kuandaa Matuta 

  • Tuta liwe na upana kati ya sentimita 90-120, na urefu wowote, [ili mradi muhudumu anaweza kutoa huduma nyingine zote kitaluni bila kukanyaga miche]. 
  • Kwatua/lima kina kirefu cha kutosha kiasi cha sentimita 15-20 ili mizizi iweze kusambaa vizuri ardhini. 
  • Choma takataka juu ya kitalu, au funika tuta kwa nailoni, majuma ili kuua vimelea vya magonjwa na wadudu. 
  • Wakati wa kuandaa, kitalu, ongeza mbolea aina ya samadi/vunde au mboji kwenye udongo kisha kwatua ili ichanganyike vizuri na udongo. 
  • Changanya kiasi cha debe 1 hadi 2 kila baada ya mita moja (hatua moja) mraba. 
  • Tuta lisiwe na mabonde mabonde au mawe mawe ambayo yanaweza kuzuia usambaaji mzuri wa mbegu kwenye tuta, lisawazishwe vizuri ili kuhakikisha usambazaji mzuri wa mbegu na kuepuka mbegu kufukiwa chini mno kiasi ambacho hazitaota. 

4. Faida na Hasara za Matuta yaliyotajwa hapo juu Matuta ya kunyanyulia udongo (raised seed beds); 

– matuta ya namna hii huruhusu maji, hewa na mizizi kupenya kwenye udongo kwa urahisi zaidi. 
– Mazao ya mizizi hupata nafasi ya kutosha kutanuka haraka zaidi 
– Matuta haya hayatuamishi maji kama mengine, hivyo hutumika zaidi kwenye maeneo yanayokuwa na mvua mara kwa mara. 

Hasara: 

Matuta ya namna hii yana sababisha sana mmomonyoko wa udongo kama hayakutengenezwa vizuri. Matuta ya makingo (sunken seed beds): 

Faida: 

1. matuta haya ni rahisi kutengeneza 
2. hutumika wakati wa kiangazi ili kuhifadhi maji na unyevu nyevu mdogo unaopatikana ardhini 
3. ni rahisi kumwagilia kwa kutumia maji ya mfereji au bomba 
4. huhifadhi unyevu nyevu kwenye ardhi kwa muda mrefu 
5. huzuia mmomonyoka wa ardhi 

Hasara: 

Matuta ya aina hii hayawezi kutumika kwenye maeneo yenye mvua nyingi. Matuta ya kawaida (flat seed beds): 

Faida: 

– ni rahisi sana kutengeneza kwani udongo ukisha kwatuliwa na kusambazwa mbegu huoteshwa 
– ni rahisi kutumia eneo kubwa kuotesha mbegu

Clothing & Apparel:

Jewelry & Watches:

Health & Beauty: