Welcome to Souq commerce Store !
MIFUMIO YA UFUGAJI WA KUKU {MADA: 03}

MIFUMIO YA UFUGAJI WA KUKU {MADA: 03}

Size :
(0 customer review)
Ipo mifumo ya aina 3 ya ufugaji wa kuku wa Asili inayotumika nchini Tanzania. Mifumo hiyo ni
Ufugaji Huria, Ufugaji Nusu Huria na Ufugaji wa Ndani. Kila mfumo una faida na hasara zake. Ni vyema mfugaji kuijua mifumo yote na kisha kuchagua anaoona ni bora kulingana na mazingira yake. Hata hivyo, katika kufanya uteuzi ni vyema kutilia maanani mfumo wenye faida zaidi na kuepuka mfumo wenye hasara nyingi.

1. Ufugaji Huria:
Katika mfumo huu, kuku huachiwa kuanzia asubuhi wakitembea kujitafutia wenyewe chakula na
maji na kufungiwa kwenye vibanda visivyo rasmi wakati wa usiku. Huu ni mfumo rahisi lakini si
mzuri kwa mfugaji wa kuku wengi kwani atahitaji eneo kubwa la ardhi.

Faida Zake:
(a) Gharama ndogo za ujenzi wa banda.
(b) Gharama za chakula hupungua kwani kuku huokota wadudu na kula baadhi ya majani.
(c) Gharama za kujenga uzio hazihitajiki.


Hasara zake:
(a) Uwezekano mkubwa wa kuku kuliwa na vicheche, mwewe na wanyama wengine, kuibwa mitaani  au kukanyagwa na magari.
(b) Kuku hutaga popote na upotevu wa mayai ni mkubwa.
(c) Kuna usimamizi hafifu wa kundi la kuku.
(d) Ni rahisi kuku kuambukizwa magonjwa.
(e) Utagaji unakuwa si mzuri kulingana na mabadiliko ya hali ya hewa.
(f) Uwekaji wa kumbukumbu si mzuri na mara nyingi kumbukumbu si sahihi.
(g)Si rahisi kugundua kuku wagonjwa na utoaji wa tiba na kinga ni mgumu.
(h) Vifaranga wengi hufa na kupotea.

Uboreshaji wa mfumo huu:
(a) Kuku wajengewe banda kwa ajili ya kulala nyakati za usiku na liwasaidie wakati mwingine
     wowote hali ya hewa inapokuwa sio nzuri.
(b) Kuku wapatiwe chakula cha ziada na maji.
(c) Kuku waandaliwe viota vya kutagia.
(d) Kuku 100 watumie eneo la ardhi la ekari moja.


2. Ufugaji Nusu Huria:
Katika mfumo huu kuku hujengewa banda rasmi na banda hilo huzungushiwa wigo (uzio) au wigo
huo hujengwa kwa mbele, ambapo kuku hulala ndani ya banda nyakati za usiku na kushinda nje ya
banda (ndani ya wigo) nyakati za mchana wakila chakula na kunywa maji humo. Mfumo huu ni ghali
kiasi kuliko mfumo huria, lakini huweza kumpatia mfugaji tija haraka sana.

Faida zake:
(a) Sehemu ndogo ya kufugia hutumika kuliko ufugaji huria.
(b) Utunzaji wa kuku ni rahisi ukilinganisha na ule wa huria.
(c) Ni rahisi kutibu na kukinga maradhi ya milipuko kama mdondo (New Castle Disease).
(d) Upotevu wa kuku na mayai ni mdogo ukilinganisha na mfumo Huria.
(e) Uwekaji wa kumbukumbu ni rahisi.

Hasara zake:
(a) Unahitaji gharama za banda na uzio.
(b) Gharama za chakula zitakuwa kubwa ukilinganisha na ufugaji huria.
(c) Matumizi ya muda mrefu ya eneo husika laweza kuwa na minyoo au vimelea vingine vyovyote
     vya magonjwa.

Uboreshaji wa mfumo huu:
(a) Fanya usafi wa eneo husika na banda kila siku.
(b) Ikiwezekana kuwe na mzunguko wa kutumia eneo hilo.

Muhimu: Ili mfugaji aweze kupata tija na mafanikio katika ufugaji wa kuku wa Asili
anashauriwa atumie mfumo huu.


3. Ufugaji wa Ndani:
Katika mfumo huu, kuku hujengewa banda rasmi na hufugwa wakiwa ndani huku wakipatiwa
chakula, maji na kufanyiwa huduma nyingine muhimu wakiwa humo ndani kwa muda wote wa
maisha yao. Kwa mfumo huu, kuku huwekwa kwenye mabanda ambayo sakafu hufunikwa kwa
matandiko ya makapi ya mpunga, takataka za mbao (takataka za randa), maganda ya karanga au
majani makavu yaliyokatwakatwa.


Faida zake:
(a) Mfumo huu unahitaji eneo dogo la kufugia hivyo ni mzuri kwenye maeneo yenye uhaba wa
ardhi.
(b) Uangalizi wa kuku ni mzuri na rahisi.
(c) Ni rahisi kuhakikisha ubora wa chakula.
(d) Hakuna haja ya kufagia vinyesi vya kuku kila siku.
(e) Kuku wanakingwa na hali mbaya ya hewa na maadui wengine.
(f) Ni rahisi kukinga na kutibu maradhi ya kuku.
(g) Uwekaji wa kumbukumbu ni rahisi.
(h) Ni rahisi kudhibiti upotevu wa kuku, vifaranga na mayai.

Hasara zake:
(a) Uwezekano wa kuku kudonoana na kula mayai ni mkubwa kama utunzaji utakuwa duni.
(b) Uwezekano wa kuku kuatamia mayai bila mpangilio ni mkubwa.
(c) Ujenzi wa mabanda na ulishaji una gharama kubwa.
(d) Mahitaji makubwa ya nguvu kazi.
(e) Kuku watakosa mionzi ya jua ambayo ni muhimu kwa kutoa vitamini D.
(f) Ni rahisi ugonjwa kuenea haraka unapoingia kwenye kundi.
(g) Muhimu: Kutokana na uwezo mdogo wa uzalishaji kimaumbile, kuku wa asili hawataleta tija
(h) kwa mfugaji iwapo atatumia mfumo huu.

Uboreshaji wa mfumo huu:
(a) Hakikisha utunzaji mzuri wa matandiko na usafi wa banda ili kupunguza unyevunyevu na joto
      kali ndani ya banda.
(b) Kuku wawe na nafasi ya kutosha, mita mraba moja hutosha kuku 5-8.

Je, ungependa kuanza ufugaji wa kisasa wa kuku wa kienyeji sasa?
Usikose.........Mada ya 4: Maandalizi ya Ufugaji Kuku wa Asili

Clothing & Apparel:

Jewelry & Watches:

Health & Beauty: